Tunaishi katika dunia yenye maudhi na machungu mengi na hakuna mtu ambae Hajawai kukwazika maishan.ukiwa bado hai,tegemea mambo mengi na ingawa kila mtu anawaza mafanikio,ni vizuri kujua kua sio kila siku mipangilio tunayotaka
Itatimika kama tulivyopanga. Kila kitu kinachotuzunguka lazima kitatukwaza kwa namna moja ama nyingine na kukwazika sio vibaya ila kushindwa kutoka katika
Hiyo hali ya kukwazika ndio JELA la watu wengi.kuna vijana wengi ambao wangekua mbali kimaisha lakini kwasababu wameshindwa kusahau yaliyowatokea,wamejikuta wakiishi maisha ya jana na sio ya leo. hakuna alie na uhakika wa milele na hivyo unatupaswa kama vijana kuacha na kusahau yasiyo ya msingi na kukumbatia yale yatakayo tusaidia kufikia ndoto zetu.vijana ni wakati wetu wa kusimama na kutoka katika maisha ya kujilaumu na kuanza kuishi maisha yenye mpango.leo ndio naanza,na jiunge nasi tena siku ijayo ambayo ntakua nafanya muendelezo ya Sahau yaliyopita ukumbatie yajayo. pia kwa wenye kupenda ushauri unaweza kuwasiliana nasi na tupo tayari kukusaidia kimawazo. kwa mawasiliano au kujua zaidi.....
Facebook page: Elly David Tanzania
Email address:vijanatzdaima@gmail.com
Tel:0688 440029
Post a Comment