Tundaman amedai kuwa atarekodi wimbo na kundi la muziki wa Kwaito, Big Nuz lenye makazi yake Durban nchini Afrika Kusini.

Big Nuz
Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, Tundaman amesema yupo nchini Afrika Kusini kurekodi ngoma na kufanya video. Msanii huyo amesema beat ya wimbo atakaowashirikisha Big Nuz umetayarishwa na Mesen Selekta na akirudi atakuja na wimbo uliokamilika.

Akiwa jijini Durban, muimbaji huyo amesema ameamua kufanya video ya wimbo wake ‘Mapenzi Yale Yale’ baada ya kupenda mazingira ya huko.

Post a Comment